MASHARTI YA LESENI YA BIASHARA

1. Mfanya biashara anatakiwa kufika mwenyewe katika Baraza la Manispaa Magharibi “A” kwa lengo la kukata Leseni.
2. Anatakiwa kukata leseni kufuatana na muda uliopangwa kisheria.
   a.Kuanzia mwezi wa Januari hadi Mei ni kipindi cha hiari cha kukata Leseni.
   b. Baada ya muda huo wakaguzi wa Baraza la Manispaa Magharibi “A” watakua na haki ya
        kukagua leseni wakati wowote baada ya kutolewa Tangazo.
  MFANYABIASHARA ATALAZIMIKA KUJIEPUSHA NA MAKOSA YAFUATAYO:-
i.                    Kufanya biashara bila ya kuwa na leseni.
ii.                  Kutumia leseni ya biashara eneo lisilo husika.
iii.                Kushindwa kuonyesha leseni ya biashara kwa wakaguzi.
iv.                 Kushindwa kuweka leseni pahali pawazi.
v.                   Kushindwa kukabidhisha leseni kwa mamlaka husika.
vi.                 Kutoa taarifa zisizo sahihi wakati wa kuomba leseni.
vii.               Kushindwa kutekeleza masharti ya leseni.
viii.             Udanganyifu wa ulipaji wa ada ya leseni.
  c. Leseni itakayokatwa zaidi ya mwezi wa Mei itaambatana na Faini ya Asilimia Thelathini (30%) na Faini ya Asilimia Hamsini (50%) kwa Fomu.
3. Ada ya Leseni ikithibitishwa na AFISA anaehusika haina Mapatano ya bei.
4. Ni kosa la kikatiba kufanya biashara  kwa  kutumia ubaguzi  wa kabila, rangi, jinsia, jimbo, dini au chama cha siasa chini ya ibara ya 12 ibara ndogo (2) ya katiba Zanzibar  ya 1984.
5.Hakikisha leseni ya biashara inakuwepo katika eneo la biashara saa zote.
6. kutokuweka leseni katika eneo linalohusika ni kosa la kisheria na faini yake ni Shilingi 30000/= za Kitanzania.
7.Hakikisha kuwa unalipa ada ya usafi wa mazingira kwa wakati unaostahiki (kila mwezi)na kuhakikisha kua eneo la nje na ndani la kufanya biashara linakuwa safi (ni jukumu la mfanya biashara kuhakikisha anasafisha na kulima eneo linalozunguka biashara yake)
8. Hakikisha Fomu yako inaambatanishwa na vielelezo vinavyohusika kwa biashara zinazohusu ruhusa au uthibitisho  wa Taasisi nyengine, biashara hizo ni kama maduka ya nyama, maduka ya dawa baridi, maduka ya Gesi, Kampuni, Vituo vya Afya, Skuli n.k.

MENGINEYO KUTOKANA NA SHERIA/ KANUNI ZA AFYA NA MAZINGIRA.
9.Kufuata sharia/kanuni zote zinazohusu Afya na Mazingira
10.Kuwepo na mpangilio mzuri wa Bidhaa katika eneo la Biashara kwa kutenganisha bidhaa za chakula na  bidhaa zisizo lingana kwa  mfano Sabuni , Mafuta ya taa, Viatu n.k.
11.Kupima na kuchunguza Afya yako  ili kuthibitishwa  kuwa unafaa kiafya kwa wale wauza migahawa, Bekari, Bucha, kiosk n.k pamoja na kuvaa sare sare maalumu wakat wa kutoa huduma zilizowekwa na kitengo cha Afya.
12.kudumisha usafi muda wote katika eneo la biashara, pamoja na vyombo vinavyotumika kutoa huduma ya biashara kwa faida ya mfanya biashara na wateja pia.
13.Kwa wafanya biashara ya vyakula vilivyopikwa hairuhusiwi kutumia vyombo vilivyovunjika (vyenye mapengo au nyufa) na vyombo vya plastiki nyepesi.
14.Siruhusa kuuza GOLOLI za kuchezea watoto na kuchezesha gemu (Video games).
15. Siruhusa kuuza dawa za Hospitali katika maduka ya vyakula,
16.Watoto chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kufanya Biashara.
17. Siruhusa kuweka dukani na kuuza bidhaa zilizoharibika (Expired).
18. Siruhusa kuuza mifuko ya Plastiki.awa



No comments:

Post a Comment

Facebook

Recent Comments

Recent Post